Thursday, June 11, 2015

Mh Lowasa aendelea kufunika aondoka na wadhamini 7014


Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa aliyetangaza nia ya kugombea urais nchini Tanzania leo amewasili katika mkoa wa Shinyanga kutafuta wadhamini ambapo maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamejitokeza kumpokea na kupata wadhamini 7014.

Pichani ni Mheshimiwa Edward Lowassa akishuka kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Ibadakuli mjini Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakimpokea Mheshimiwa Edward Lowassa.


Mheshimiwa Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM
Mheshimiwa Edward Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kumpokea nje ya jengo la NSSF zilipo ofisi za mkoa za CCM mjini Shinyanga.

Miongoni mwa wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kumdhamini Mheshimiwa Lowassa.


Wadhamini wa Lowassa wakipunga mkono katika ukumbi wa NSSF

Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge akiwapungia mkono wakazi wa Shinyanga waliojitokeza kumuunga mkono mheshimiwa Edward Lowassa.


Mheshimiwa Edward Lowassa akisalimiana na watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga waliojitokeza kumdhamini.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akiwasilisha orodha ya majina ya wadhamini 7014 kwa waziri mkuu wa zamani Lowasa, idadi hiyo ya wadhamini wote ni wanachama hai wa CCM kutoka katika wilaya zote za mkoa huo ambao kwa hiyari yao na mapenzi waliyonayo wameamua kumdhamini .


Mheshimiwa Edward Lowassa akiwashukuru watanzania waliojitokeza kumuunga mkono ambapo amesema katika mikoa yote aliyopita hajawahi kupata idadi kubwa ya wadhamini kama ilivyotokea Shinyanga kwa kupata watu 7014 waliojitokeza.

Waziri mkuu wa mstaafu Edward Lowasa ambaye anaomba ridhaa ya chama chake kuteuliwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, amesema katika mikoa yote aliyopita hajawahi kupata idadi kubwa ya wadhamini kama ilivyotokea Shinyanga kwa kupata watu 7014 waliojitokeza.

Mheshimiwa Edward Lowassa akiwa na makatibu kata wa CCM aliowahi kufanya nao kazi mkoani Shinyanga miaka iliyopita.
Wakazi wa Shinyanga wakimpungia mkono mheshimiwa Edward Lowassa.

No comments:

Post a Comment