SERIKALI IWEKE KIPAUMBELE KWENYE LISHE
NaGodfrrey thomas
Serikali imetakiwa kuweka vipaumbele katika masuala ya lishe
ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo yanayosababishwa na lishe duni
hivyo kuathiri maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Katibu Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (ANGONET)
,Petter Bayo amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya lishe nchini na kuongezeka
kwa udumavu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano 5 hadi kufikia asilimia
42% ya watoto hao kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2012.
Bayo alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa habari
amesema kuwa iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa
athari zitakua kubwa katika shughuli za uzalishaji kutokana na lishe duni na
pia kuathiri Nyanja za elimu na sekta mbali mbali kuwa hayo jana akizungumza na Waandishi wa habari.
“Lishe ni kiini cha maendeleo ya jamii yoyote ile na nchi
yoyote ile ni vyema serikali ikatilia mkazo suala la lishe kwani ni kichocheo
muhimu cha maendeleo kwa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi hasa waishio
vijijini” Alisema Bayo
Mratibu wa Angonet ,Petro Ahham alisema kuwa Serikali
inapaswa kutupia macho suala la upatikanaji wa chakula na kuangalia uhaba wa
chakula unaoweza kusababisha watu kufa kwa kukosa chakula.
Ahham anaeleza kuwa ukosefu wa madini chuma kwa watoto umekua
ukisababisha ugonjwa wa Anemia unaowapelekea watoto kusinzia wakiwa mashuleni
hata kuchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu
kutokana na Lishe duni.
Mwanachama
wa Angonet ,Jovitha Mlay anaeleza kuwa shirika hilo kwa sasa linashirikiana
Umoja wa mashirika yanayojihusisha na masuala ya lishe Tanzania (PANITA) katika kutoa elimu
juu ya lishe na kufanya uhamasishaji mashuleni na katika makundi mbalimbali ya
jamii husasan kwenye Kanda ya Kaskazini,mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara.
No comments:
Post a Comment