Waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ametangaza rasmi nia ya kuwania urais wa kupitia chama cha mapinduzi CCM.Leo jijini Arusha
Mbunge
wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa ametangaza rasmi
nia ya kuwania urais wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi mbele ya
umati wa watu waliofurika uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha na
kutaja vipaumbele vyake kuwa ni elimu,kupambana na umaskini,kulinda
rasilimali za nchi na kuwaunganisha watanzania .
Mh.Lowassa ambaye aliingia.uwanjani akisindikizwa na msafara wa
pikipiki na magari pia amesema akipewa fursa atahakikisha anadumisha
muungano.
Amesema ataweka misingi imara ya kuharakisha maendeleo mazuri kwa
wananchi na kuwawezesha vijana kuondoa tabaka la walionacho
nawasionacho.
Awali viongozi wa dini na siasa akiwemo Kkingunge Ngombale Mmwiru
wameseama Lowassa ana sifa za kiongozi anayefaa kuliongoza taifa kwa
sasa.
Sherehe hizo zilizohudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka kona
mblimbli nchini burudani kubwa ilikuwa ni Helkopta ya Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Geita Bw. Joseph Msukuma.
No comments:
Post a Comment