Wema Sepetu aanza safari ya kuwania Ubunge wa Viti maalum Singida
Tanzania
2006 na Msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu akipokea maelekezo kutoka
kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi,Bwana Alluu Ismaili Segamba kabla ya
kuongea na wananhi pamoja na wanachama waliohudhuria kwenye mkutano huo.
Hatimaye
aliyewahi kuwa, Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Wema Spetu
ameanza safari maalum ya kuwania nafasi ya Ubunge kupitia chama cha
Mapinduzi Mkoani Singida, ambapo ni chimbuko la Mama yake Mzazi
.
Wema
yupo aliwasili Mkoani Singida huku akifanya harakati mbalimbali za
kichama ikiwemo uhamasishaji wa Wananchi kujiandikisha katika daftari
la wapiga kura.
Segamba alitoa kauli hiyo kwenye mkutano huo na kufafanua
kuwa hali ya shule ya sekondari Ikungi hivi sasa ni mbaya sana kutokana
na wanafunzi pamoja na walimu wao kutokuwa na sehemu za kujisaidia
kufuatia viongozi na wazazi wa shule hiyo kushindwa kujenga matundu ya
vyoo kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo.
“Akazungumza
Sigamba na magamba sijui na kitu gani tumeenda shule,kwanza nikiri ni
kweli nimeenda kwenye shule ya sekondari ya Ikungi nimekula chakula na
wanafunzi na walimu,lakini hali ya shule ya sekondari ya Ikungi ni mbaya
shule itafungwa kwa kukosa vyoo”alisema kwa kujiamini Segemba.
“Kama
wazazi mpo hapa,kweli siyo kweli…kweliii,shule itafungwa pale kwa
kukosa vyoo halafu mna mbunge anakataza michango,sasa pale naenda
kujisaidia mimi au watoto wenu?”alihoji katibu huyo huku akionyesha
kukerwa na hali hiyo.
Alisema
shule kukosa vyoo ni suala la aibu wanafunzi pale wa kidato cha nne na
tano hawana pakujisaidia,halafu anakuja kulalamika kuwa katibu wa CCM
ameenda pale shuleni kutafuta kura,jambo ambalo hakuwa tayari
kukubalinanaalo.
Naye
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ikungi (MNEC),Jonathani Njau
aliwakumbusha wakazi wa kata ya Ikungi juu ya umuhimu wa kujitokeza kwa
wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura,ili wakati
ukifika wajitokeza pia kupiga kura.
“Lakini tunatakiwa tukajiandikishe kwa wale ambao tuna sifa
ya
kupiga kura,kwani watu wengi wanadhani zoezi la kujiandikisha ni la
kisiasa siasa tu,la mzahamzaha si kweli.”alisisitiza mjumbe huyo.
Hata
hivyo Njau pamoja na kutokuwepo kwa mikakati yeyote madhubuti ya
kulirudisha jimbo hilo kutoka CHADEMA,lakini alijikuta akitamba kuwa
mwaka huu CCM bado kitashinda na hapo Ikungi ndiyo watashinda zaidi.
“Kama
mlidanganywa zile sarakasi za 2010 mwaka huu hakuna,hazitakuwepo na
rafiki zangu,nawabip vijana wa Ikungi kuwa uhuni mlioufanya mwaka
2010,mwaka huu mlie tu,CCM ya mwaka huu imejitosheleza”alisisitiza Njau.
Msanii
wa Bongo Movie na Miss Tanzania 2006,Bi Wema Sepetu katika mapokezi yake
alipofika kwenye viwanja vya ghala ulipofanyika mkutano wa hadhara.
Miss
Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Wema Spetu(wa pili kutoka
kushoto) akishiriki kuimba wimba wa kimila mara baada ya kukaribishwa
kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili ya kuwahamasisha
wananchi kujiandikisha
No comments:
Post a Comment