Katika taarifa yake Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Krismass na mwaka mpya kwa gharama za Serikali mwaka huu.
Balozi Sefue ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo afanye kwa gharama zake mwenyewe.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa imesema fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji wa uchapishaji wa kadi hizo zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, idara na Taasis za umma zinadaiwa na wananchi waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine.
Angalizo hilo lililotolewa hili hapa
No comments:
Post a Comment