G Nako apoteza dola Elfu tatu za kimarekani.
Rapper anayeunda kundi la Weusi G.Nako ametoa taarifa ya kupotelewa
na pesa takribani dola elfu tatu ambazo ni zaidi ya shillingi milioni 6
za kitanzania wakati walipokuwa kwenye kikao cha wasanii
.Akithibitisha
upotevo wa kiasi hicho cha pesa msemaji wa kampuni ya weusi rapa Nikk wa
Pili amebainisha kuwa bado hawana uhakika kama ni mtu ameiiba au
zilidondoka lakini pia G.nako mwenyewewe haamini kama ni mtu
alimchomolea kwa kuwa alikuwa amekaa na watu wake wa karibu ambao sio
rahisi kumfanyia kitendo hicho.
Taarifa zinasema kuwa msanii huyo
aligundua upotevu wa pesa zake akiwa tayari akiwa ameondoka eneo la
tukio kitu kilichomfanya arudi eneo hilo na kukuta bahasha aliyohifadhia
pesa hizo ikiwa tupu.
Na kuhusiana na uvumi kuwa pesa hizo zilikuwa ni za rapa mwingine wa
kundi hilo la weusi John Makin,Nikki wa pili amekanusha na kusema kuwa
pesa hizo zilikuwa za biashara binafsi za G.Nako na alikuwa anaenda
sehemu kufanya malipo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment