Sunday, April 24, 2016

Picha 5 za mwanzo mwisho uzinduzi wa Tmasha la filamu la kimataifa la Tanzanite












Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa michezo nchini,Nnape Nnauye ametaja mambo manne ambayoni vikwazo ndaniya sekta ya sanaa filamu nchini na kuyaita ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha  2016/17.

Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni
uporaji wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu
ya kazi za wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu
nchini sanjari na tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi
za wasanii nchini. 

Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na
wasanii maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba
jipu la kwanza ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi
za wasanii nchini.

“Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka
2016/17 ni uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi
wananyonywa jasho lao”alisema Nnape

No comments:

Post a Comment