Sunday, June 12, 2016

ACT baada yakunyimwa kufanya mkutano imeamua haya!!!



Baada ya Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa,
Chama Cha ACT- Wazalendo kilipanga kufanya kongamao Jumapili ya June 12
2016 kwa lengo la kujadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017.

Taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Mwenyekiti wa
chama hicho Anne Mghwira imesema kwamba kongamano hilo lililenga kumpa
fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo
angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani
kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida walipewa taarifa na
mwenye ukumbi (LAPF Millenium Tower) kwamba polisi walikuwa wametanda
katika eneo la ukumbi tangu saa kumi na mbili asubuhi na ilipofika saa nne
kamili asubuhi mwenye ukumbi aliwataarifu rasmi kuwa amepewa taarifa na
kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni kwamba chama chao hakina kibali
cha kufanya kongamano hilo na hivyo asiwafungulie ukumbi huo.

Hivyo kupitia taarifa hiyo chama ACT-Wazalendo kimesema kimesikitishwa
sana na hatua hiyo ya polisi na wanaitafsri kuwa ni mwendelezo wa hatua za
uhakika katika kufifisha demokrasia katika nchi.

No comments:

Post a Comment