Sunday, November 13, 2016

DAS Arusha pamoja na viongozi wa shirikisho walivyozungumzia mikopo ya elimu ya juu



Katibu tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amekutana na wanafunzi wa  shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu nakuwataka vijana kutengeneza vikundi pamoja nakubuni mawazo yatakayosaidia kuwesha kupata fedha zilizotengwa na serikali milion 445 za wanawake na vijana  hasa katika serikali ya awamu ya tano ya viwanda

Hata hivyo Shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu imesema tayari serikali imeshapeleka mikopo kwa wanafunzi zaidi ya bilion 71 baada yakutoa siku saba kuitaka serikali kutoa mikopo

Katibu msaidizi wa shirikisho la elimu ya juu amesema Daniel Zanda amesema jumla ya wanafunzi wasiopungua 25700 wameshaanza kupatiwa nakuiomba serikali kuhakiki suala la umri nakubaini wanafunzi hewa kwenye baadhi ya vyuo

No comments:

Post a Comment