Friday, November 11, 2016

Maamuzi ya mahakama kuhusu dhamana ya Lema


Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema leo amerudishwa rumande baada ya upande wa jamhuri kutoa hoja zakukata rufaa iliyopelekea kukosa dhamana

Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha  aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha alikuwa amefikia hatua yakutoa dhamana  lakini upande wa jamhuri ulileta hoja hiyo  ambapo  hakimu Kamugisha  alikubaliana  kusitisha dhamana hiyo  hadi pale upande wa jamhuri utakapokata rufaa

Wakili wa chadema Shedrack Mfinanga amesema baada ya hakimu kutoa uamuzi huo wataendelea kusubiri nakufuatilia ili waweze kuamua kuhusiana na hatua watakazochukua juu ya rufaa hiyo

No comments:

Post a Comment