Tuesday, January 17, 2017

Kada CCM amfagilia Magufuli amponda Lowasa

KADA CCM AMFAGILIA MAGUFULI,AMPONDA LOWASA





Ninaweza kukuhakikishia kwamba taswira na mtazamo wa Mwalimu Nyerere sasa inajitokeza dhahiri kwa Rais Magufuli."Na wale wanaodhani kwamba, haya anayoyafanya ni nguvu ya soda inayotokana na msukumo wa uchaguzi au upinzani, watakuja kushangaa sana.JPM ni mtu ambaye ndani ya miaka 10 ataonesha njia kuhusu uongozi bora na uliotukuka katika eneo hili la Afrika Mashariki,Afrika,na Dunia. Mimi si mtabiri wa Kiyahudi wala sina uhusiano nao lakini angalia hali itakavyokuwa baada ya miaka 10."Sio Mimi wakwanza kumsifia na kumpongeza Mh.Rais MAGUFULI,Maraisi mashuhuri Ulimwenguni kote,wanaunga mkono Juhudi za Mh RAIS (JPM),katika adhima ya kuutangazia UHURU uchumi wa Tanzania kutoka mikononi mwa wanasiasa,Mafisadi, Walafi wa Tumbo zisizo na shukrani.Matumbo yao yamejaa maendeleo ya watanzania ambao kovu na kidonda cha umasikini bado chungu inayofutwa kwa kasi kubwa na Mh Raisi   JPM.

Mh.Raisi,Magufuli amechukua njia sahihi ambayo naamini si muda mrefu Watanzania wataanza kunufaika na matunda ya uongozi wake.Rais Magufuli amedhihirisha kwamba yeye kauli yake ni kutenda kazi na amedhihirisha kwamba uongozi mzuri ni utumishi si usultani. Kwa hivyo kwa Watanzania wengi na wadadisi wengi hizi ni hatua ambazo lazima zishabikiwe na kusifiwa lakini pia kumtia na kuunga mkono Juhudi hizi za Serikali ya awamu ya Tano.hasa kwa Taifa kama Tanzania.

Rais Magufuli amechukua hatua kali ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kwa nguvu zake zote, jambo ambalo wananchi wengi wa kawaida walitegemea kuliona kwa rais wao mteule na kwamba hilo litaisaidia sana Tanzania kupiga hatua za kimaendeleo Haraka sana.Kwa sasa Tanzania SIO shamba la Bibi,Bali ni Shamba Darasa.

Rais Magufuli kushiriki katika shughuli za kijamii na usafi ilimaanisha pia kwamba yuko tayari kuisafisha Tanzania nzima dhidi ya ufisadi na kuhakikisha wananchi wanaishi maisha mazuri.Kwa mtazamo wangu,Raisi Magufuli Hakushiriki USAFI wa kufagia maganda ya Ndizi yaliooza,Bali ilikuwa ni ishara ya kuisafisha Tanzania na mfumo uliooza ili iwe mahali salama pa kuishi."Raisi anaongoza kwa mifano na anafundisha.Lazima tuwe safi,UCHAFU MWIKO utafagiliwa.Ndio maana baadhi ya uchafu umeanza kusafishwa.

Rais Magufuli ameonesha Unyerere na Unkrumah na nina hakika kwamba atawadhihirishia watu kuwa yeye ni mtu mwenye azma njema na Watanzania. Tanzania itakuwa nchi ya kupigiwa mfano katika siku za usoni na kujifunza ndio maana nasema "Tanzania ni Shamba Darasa"

Miongoni mwetu wapo ambao wanatarajia kuwania uongozi wa kisiasa kwa gharama yoyote ile kwa kaulimbiu zozote zile ,Na wengi wakidiriki kuvihama vyama vyao vilivyowalea ili Tu kutafuta madaraka,wengine wakienda kwa waganga wa kienyeji na wangine wakiamini Tabili za TB JOSHUA

Lakini swali la msingi la kujiuliza ni hili: Kwa nini unataka kuongoza? "Katika Afrika has a Tanzania, njia nyepesi ya kupata utajiri wa harakaraka ambao huwezi kuutolea maelezo namna ulivyopatikana ni kuingia katika uongozi wa kisiasa. Kama unataka kupata utajiri bila kuufanyia kazi kwa namna yoyote basi ingia kwenye siasa za Afrika.

"Huo ndio ukweli, nenda kila mahala Afrika isipokuwa kwa watu wachache sana.

 Mtu pekee anayeonekana kwa sasa Mbinguni na Duniani la kutumikia wananchi na siyo kutafuta utajiri ni Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli pekeee.Ninasema pekee kwa sababu yeye ni chaguo la Mungu.

Waliobaki katika Afrika has a Tanzania... Sujui... Mtanisamehe Viongozi wetu wengi wa CHADEMA,CUF,NCCR,UKAWA nk, wanawinda na kutaka uongozi ili kujikusanyia majumba, magari na pesa na hiyo ndio maana vyama ya upinzani Tanzania has a CHADEMA hauwavutii watu na wananchi kabisa, wanaume au wanawake,kwa sababu vipaumbele vyao nimevitaja hapo juu.

Na kwa bahati mbaya sana,hata wafuasi wao wa CHADEMA  Hununuliwa kwa pesa, na sina hakika kama Siku ya kupiga kura,huchagua tofauti.
Wapiga kura wao nao wanatazamia kuhongwa au kununuliwa na wagombea wa CHADEMA au UKAWA ili waweze kuwapigia kura.

Kama Tanzania haitapambana na ukabila (kuchagua mtu kwa ukabila) na rushwa, basi tujue kwamba Tanzania halitaweza kamwe kupata viongozi wazuri.Ndio maana Mh.RAIS alianza kusafisha serikalini,sasa anasafisha ndani ya CCM huku kote kulikuwa na uchafu.Swali langu la msingi.LOWASA,MBOWE,SAIF,LIPUMBA nani atawasafisha??????

Tunaishi katika siasa ambayo tunawapigia makofi na kuwashangilia wezi,mafisadi lakini tunawanyanyasa watu wazuri na kuwabeza kama Mh.RAIS  ,JPM

Ilifika mahala hata madaktari ambao tumewasomesha lakini tunapokuwa wagonjwa, hasa tabaka la wanasiasa, tunakimbilia London kwa kuwa tukuwa hatuna imani na madaktari wetu wala hospitali zetu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba rushwa ilikuwa imekita mizizi katika mfumo wetu wa maisha kiasi kwamba hatuwezi kufikiria hali za hospitali zetu za Taifa.Mh.RAIS JPM ,amejikita kurudisha imani ya Huduma na Mali zetu ili tunufaike wote.

Narudia kusema tena,Tunachagua wezi kwa kuzingatia ukabila au ukubwa wa pochi zao (pesa) na bado tunatarajia wafanye mema. Haiwezekani.  "Kiongozi mzuri na makini lazima atambuliwe kwa uwezo na uzuri wake na kiongozi dhaifu lazima atambuliwe kwa udhaifu wake."

Tumekuwa na tabia tunachagua wezi, fisi ili wawalinde mbuzi lakini wakati mbuzi wetu wanapoliwa na hao mafisi tunashangaa. Tunashangaa nini?" Kumufikiria Lowasa,Mbowe,Lema na UKAWA kwa siasa za hapa ndani ni sawa na kukabidhi FISI kulinda MBUZI,siku wakiliwa tusishangae.

Nawashukuru sana kwa kusoma Makala yangu.Tanzania ya JPM ni shamba Darasa.

Written & Edited by

NETHO NDILITO
(Hard working & God Fearing Servant)
27.12.2016
0622738001

No comments:

Post a Comment