Leo asubuhi nimefanya mazungumzo na Kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza Ndg. Jeremy Corbyn katika Ofisi ya Jimboni kwake Islington Kaskazini.
Tumezungumza kuhusu ujenzi wa Ujamaa duniani katikati ya wimbi la siasa Kali za mrengo wa kulia zinazoendelea sasa.
Pia tumejadiliana wimbi la kubana uhuru wa mawazo na demokrasia Afrika na Tanzania hususan.
Nimempa rasmi mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kidemokrasia wa kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha utakaofanyika jijini Arusha tarehe 25 Machi 2017. Chama cha Labour kimekubali kuhudhuria mkutano huo.
Ndg. Corbyn pia amenialika kwenye mkutano mkuu wa Labour ambapo Seneta Bernie Sanders atahudhuria pia.
Zitto Z Kabwe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment