USALITI CCM: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Sophia Simba amefukuzwa uanachama kwa kosa la usaliti, Adam Kimbisa na Dk Emmanuel Nchimbi wapewa onyo.
ORODHA KAMILI YA WALIOFUKUZWA CCM DODOMA LEO 11/03/2017
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma ambapo Mkutano Mkuu unaendelea ni kwamba, baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali. Onyo kali alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne.
Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika. Hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.
Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga Ernest Kwirasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Nesta Msabatavunga, Mjumbe wa Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.
Pia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido Leiza amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Molleli, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Hawadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC Gureta.
Waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye amepewa onyo kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha, Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC Tunduru, Cheif Kalolo ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali.
No comments:
Post a Comment