Ugeni
huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali
duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership
utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi
katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza
utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
“Hoteli
na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa
ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.
Rais
Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na
maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili.
Mbali ya ujio huo,
wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush,
mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria
mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.
“Jiji
la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja
kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna
watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu
mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na
baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema
katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar
es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa.
Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya
Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda
Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.Wasafiri wa mikoani wataathirika
zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo
ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais
Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi
kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria
yatakayokuwa yanatoka
chanzo http://peruzibongo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment