Wednesday, November 26, 2014


 Ile ripoti ya CAG kuhusu ishu ya Escrow imewasilishwa, iko hapa unaweza kuisoma

 
 mwenyekiti wa kamati ya pac Zitto kabwe
 


Ile ripoti ya CAG kuhusu ishu ya Escrow imewasilishwa,


Katika kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe waliwasilisha Ripoti ya ishu ya Escrow ambapo kama hukupata kusikiliza wakati Ripoti hiyo ikiwasilishwa hii ni sehemu ya uwasilishwaji wa Ripoti hiyo.

“…Katika fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya viongoozi wa kisiasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.
Kwa upande wa Viongozi wa Kisiasa walioingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mheshimiwa Andrew Chenge Mbunge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi Bil. 1.6, mheshimiwa Anna  Tibaijuka Mbunge na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, shilingi Bil. 1.6, Mheshimiwa William Ngeleja Mbunge na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, shilingi milioni 40.4, ndugu Daniel Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4, ndugu Paul Kimiti, ambaye ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4 na ndugu Enos Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCo aliingiziwa shilingi milioni 161.7…“– Zitto Kabwe.
Kwa upande wa Majaji,  Profesa Eudis Ruangisa aliingiziwa shilingi milioni 404, Mheshimiwa Mujulizi milioni 40.4.
Kwa upande wa Viongozi wa madhehebu ya Kidini walioingiziwa fedha ni Askofu Methodius Kilain shilingi Milioni 80.9, Askofu Nzigirwa milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Simon milioni 40.4..”– Zitto Kabwe.
“… Kamati imependekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha afikishwe Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha za umma…“– Deo Filikunjombe.
Kwa upande wa Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili baada ya kupitia vielezo vilivyomo kwenye ripoti ya CAG kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa Waziri Mkuu  alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchota  fedha kwenye akaunti ya Escrow, ushahidi ulioletwa mbele ya kamati  za ofisi ya CAG ulionyesha kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa juu ya jambo hili na kamati imethibitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua yoyote kuzuia mhamala huu usifanyike…“– Deo Filikunjombe.
Kamati kwa kuzingatia kielelezo namba 22 inathibitisha kwamba bila shaka Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri sana na kwamba aliridhia mhamala huu usifanyike, ndio maana katika maelezo yake  ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alilithibitishia Bunge kuwa fedha za ESCROW hazikuwa fedha za umma…”– Deo Filikunjombe.

No comments:

Post a Comment