Wavaa vimini wacharazwa bakora..!!
Viongozi wa Kitongoji cha Kasalazi
kilichoko katika Kijiji cha Kanyara wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza,
wanadaiwa kuwachapa fimbo hadharani wanawake wanaovaa nguo fupi na za
kubana zinazoonyesha baadhi ya sehemu zao za siri.
Pia viongozi hao wanadaiwa kuwatoza faini
ya Shilingi elfu 20,wanawake wanaokutwa na nguo hizo kama njia ya
kuwafanya wasiendelee kuvaa nguo hizo.
Mmoja wa wasichana waliowahi kuchapwa na
viongozi hao aliyejitambulisha kwa jina la Juliana Mafuru, alichapwa
fimbo baada ya kufika kijijini hapo kwa lengo la kununua dagaa.
Amesema cha kushangaza ni kwamba, baada ya
kufika katika kitongoji hicho, mgambo walimkamata na kumchalaza bakora
mbele za watu nje ya boti aliyokuwa amemepanda.
Nao wakazi wa kijiji hicho Lafael Bitulo
na Mariamu Chacha, wamesema mwenyekiti wa kitongiji hicho na katibu
wake, ndiyo vinara wa tabia hiyo kwa kuwa wamekuwa wakinufaika nayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji
hicho Andrea Mkama, amekiri kuwachapa fimbo wanawake wanaovaa nguo fupi
na zinazobana kwa mavazi wanayovaa ni ya udharirishaji.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Kanyara Lazoro Mgonzo, amethibitisha wanawake kuchapwa fimbo ingawa
amesema ni kitendo cha udharirishaji.
Mkuu wa Wilaya Sengerema Zainabu Terack, alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema hana taarifa ingawa aliahidi kulifuatilia.
No comments:
Post a Comment